TCU WAFUNGUA NAFASI YA KUFANYA THIRD ROUND 2016/2017
TANGAZO KWAUMMA
Tume ya vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwaimekamilisha kuchakata maombiya kujiunga na Vyuo Vikuu naTaasisi za Elimu ya Juu kwa awamu ya kwanza na ya pili. Orodha na majina ya walichaguliwa yameshapelekwa vyuoni kwa ajili ya kuiidhinishwa na Seneti za vyuo husika. Baadhi ya vyuo vimeshaanzakuyatangaza.
Hata hivyo, kuna waombaji ambao bado wako kwenye mfumo na hawajachaguliwa kwenye koziyoyote kati ya walizoombakutokana na sababu mbalimbali kama ifuatavyo:-
· Ushindani mkubwa katika programu za masomo walizoomba ukilinganisha na ufaulu wao;
· Waombaji kushindwa kukamilisha taratibu za uombaji; na
· Waombaji kutokuwa na sifa kwa koziwalizoziomba.
Kutokana na hali hiyo, Tume inautangazia umma kuwa mfumo waudahili utafunguliwa tena kwa awamu ya tatu mnano tarehe 10 mpaka tarehe 16 Oktoba 2016 ili kuruhusu waombaji na aina hii kufanya uchaguzi upya aukukamilisha maombi yao.
Tume inapenda kufafanua kuwa programu za masomo zisizoonekanakwenye mtandao zimekwishajaa, hivyo waombaji watalazimika kuomba zile tu zinazoonekanamtandaoni.
Zoezi hili la uombaji kwa awamu ya tatu linawahusu waombaji wenye sifa za kidato cha Sita, Stashahada na sifa linganishi. Hakutakuwa na malipo yoyote kwa waombaji hawa. Tume inapenda kisisitiza kwamba, awamu hii haitawahusu waombaji wapya, ambao hawakuwahi kujisajili wala kuomba udahili kwa awamu ya kwanza na ya pili.