-->

EXCLUSIVE: Kutoka Gabon kuhusu mchezaji aliyeifunga Angola kupimwa dawa za kuongeza nguvu



Moja kati ya stori ambazo zilichukua headlines jioni ya jana Tanzania ni kuhusiana na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17  Serengeti Boys kudaiwa kuwa alipimwa na viongozi wa CAF kama alitumia dawa za kuongeza nguvu baada ya mchezo dhidi ya Angola.
Abdul Hamis Selemani ambaye ndio alikuwa karipotiwa kuwa alikwenda kupimwa kwa kushukiwa kuwa alitumia dawa za kuongeza nguvu kutokana na uwezo wake mkubwa aliounesha katika game dhidi ya Angola licha ya kutoka majeruhi na kuifungia Serengeti Boys goli la ushindi na baadae kuibuka mchezaji bora wa mechi.
mboyablog  imempata afisa habari wa TFF Alfred Lucas ambaye alikuwa Libreville Airport kujiandaa na safari ya kwenda Port Gentil “Kwanza niwatoe shaka watanzania kwamba kuchukuliwa vipimo kwamba kuna shaka kuwa mchezaji katumia dawa za kusisimua misuli au la ni utaratibu wa kawaida” >>>Alfred Lucas
VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera


Read also-: