-->

MPYA KUTOKA HESLB TAARIFA MAALUMU KWA WALIOKUWA WAMEKOSEA KUOMBA MKOPO 2016/2017

 Image result for HESLB
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imekamilisha zoezi la kurekebisha fomu za maombi ya mikopo kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017. Zoezi hilo lilianzatarehe 3 na kumalizika tarehe 7 Oktoba 2016.
Kwa sasa Bodi inaendelea na hatua za awali za upangaji wa mikopo ambapo taarifa za wanafunzi watakaopangiwa mikopo zitatolewa kwenye tovuti ya Bodi www.heslb.go.tz siku chache zijazo.
NB: Bodi inawakumbusha waombaji mikopo wote kuwamakini na watu wasio waaminifu wanaoweza kutumia fursa hii kujipatia fedha isivyo halali.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Read also-: