NACTE: VYUO VILIVYOFUTIWA USAJILI 2018/2019
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Sheria inazitaka Taasisi zote zinazotoa elimu ya ufundi kusajiliwa kabla ya kuanza kuendesha mafunzo yoyote. Hivyo, taasisi yoyote hairuhusiwi kutoa mafunzo yoyote bila kusajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). Ili kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa yanakidhi viwango, Baraza hufanya ukaguzi wa mara kwa mara vyuoni. Taratibu za kisheria huchukuliwa kwa vyuo vinavyokutwa na mapungufu au kukiuka taratibu za Baraza za uendeshaji mafunzo. Taratibu na hatua za kisheria zinazochukuliwa ni pamoja na kukitaka chuo kufanya marekebisho ya mapungufu yaliyobainika katika muda maalumu, kusitisha programu husika, au kufuta usajili wa chuo husika. Baraza linapenda kuutangazia umma kwamba matokeo ya ukaguzi wa vyuo 458 uliofanyika kuanzia Julai 2017 mpaka Septemba 2017 (uliouhusisha pia vyuo 112 vya Ualimu na vyuo saba (7) vilivyokutwa haviendelei na shughuli za elimu) yalibainisha kwamba vyuo 426 vilikutwa na vigezo vya kutoa mafunzo na vyuo 32 vilikutwa na mapungufu. Baraza limechukua hatua mbalimbali kwa vyuo 32 vyenye mapungufu kama ifuatavyo: 1.0 Kufuta Usajili Baraza limefuta usajili wa vyuo 20 baada ya kushindwa kufuata taratibu zinazoendana na matakwa ya usajili wa vyuo hivyo. Uamuzi huu umefikiwa kwa kuzingatia Kifungu cha 20 cha Kanuni za Usajili wa Vyuo vya Ufundi, 2001 (GN 279 of 26/10/2001).Vyuo vilivyofutiwa usajili ni kama vilivyoorodheshwa katika Jedwali Na. 1. Baraza limeishaviandikia barua vyuo husika kuvitaka vihakikishe kuwa wanafunzi walioko kwenye programu zinazotolewa na vyuo hivi wanahamia kwenye vyuo vingine vilivyosajiliwa na Baraza kutoa programu kama hizo. Jedwali Na. 1: Vyuo vilivyofutiwa Usajili Na. Jina la Chuo
- Covenant College of Business Studies – Dar es Salaam
- Mugerezi Spatial Technology College – Dar es Salaam
3 | Techno Brain – Dar es Salaam | ||
4 | DACICO Institute of Business and Management – Sumbawanga | ||
5 | Arusha Institute of Technology – Arusha | ||
6 | Lisbon Business College – Dar es Salaam | ||
7 | PCTL Training Institute – Dar es Salaam | ||
8 | Royal College of Tanzania – Dar es Salaam | ||
9 | Iringa RETCO Business College – Iringa | ||
10 | Highlands Health Institute – Njombe | ||
11 | East African Institute of Entrepreneurship and Financial Management (EAIEFM) – Arusha | ||
12 | Musoma Utalii College – Shinyanga | ||
13 | Mlimani School of Professional Studies – Dar-es-Salaam | ||
14 | Dinobb Institute of Science and Business Technology – Mbeya | ||
15 | Institute of Social Work – Mbeya | ||
16 | Regency School of Hygiene – Dar es Salaam | ||
17 | St. Peters College of Health Sciences – Dar es Salaam | ||
18 | Genesis Institute of Social Sciences – Dar es Salaam | ||
19 | Institute of Management and Information Technology – Dar es Salaam | ||
20 | Boston City Campus of Business College – Dar es Salaam | ||
2.0 | KUSITISHA PROGRAMU ZISIZOIDHINISHWA NA BARAZA |
Kabla ya kuanza kuendesha mafunzo ya kozi yoyote, chuo kinatakiwa kihakikishe kuwa mtaala wa mafunzo hayo umepitishwa na Baraza na Idara itakayosimamia mafunzo hayo imekaguliwa na kuonekana ina uwezo wa kuendesha mafunzo hayo katika ngazi husika. Vyuo vitatu (3) vilivyoorodheshwa katika Jedwali Na. 2 vimekutwa vikiendesha mafunzo bila kupata idhini ya Baraza; hivyo vimesitishiwa kutoa programu hizo ambazo hazikuidhinishwa na Baraza. Wanafunzi wanaosoma programu hizo zisizo na idhini ya Baraza watatakiwa kudahiliwa kwenye programu zenye idhini ya Baraza kulingana na sifa za ufaulu zinazotakiwa. Uamuzi huu umefikiwa kwa kuzingatia Kifungu cha 22 (1) cha Kanuni za Usajili wa Vyuo vya Ufundi, 2001 (GN 279 of 26/10/2001). Jedwali Na. 2: Vyuo na Programu Zilizositishwa
Na. | Chuo | Programu | |||
1 | Quality Development College – Masasi | Medical Attendant | |||
2 | St. Glory Nursing School – Dar es Salaam | Medical Attendant and Medical Laboratory Sciences | |||
3 | Lake Victoria Disability Medical Training | Nursing and Midwifery | |||
Centre – Mwanza | |||||
2 3.0 VYUO VILIVYOZUILIWA KUDAHILI WANAFUNZI WAPYA Jumla ya Vyuo tisa (9) vimesitishwa kudahili wanafunzi wapya kuanzia mwaka wa masomo 2018/2019. Uamuzi huu umefikiwa kwa kuzingatia Kifungu cha 22 (1) cha Kanuni za Usajili wa Vyuo vya Ufundi, 2001 (GN 279 of 26/10/2001). Hata hivyo, wanafunzi waliopo waliodahiliwa kwenye vyuo hivyo wanaruhusiwa kuendelea na masomo kama kawaida mpaka watakapohitimu mafunzo yao. Orodha ya vyuo hivyo ni kama inavyoonekana kwenye Jedwali Na. 3. Jedwali Na. 3: Vyuo vilivyosimamishwa kudahili wanafunzi wapya mwaka wa masomo 2018/2019
Na. | Jina la Chuo |
1 | Montfort Business College – Dar es Salaam |
2 | Institute for Environment and Development Sustainability – Dar es Salaam |
3 | Songea Clinical Assistant Training Centre – Songea |
4 | Institute of Continuing and Professional Studies – Zanzibar |
5 | Tanzania Institute for Trade and Investment – Dar es Salaam |
6 | Institute of Research and Innovation Zanzibar – Zanzibar |
7 | Silva Business and Management – Dar es Salaam |
8 | Mbeya Polytechnic College –Tukuyu Campus |
9 | Earth Science Institute of Shinyanga – Shinyanga |
IMETOLEWA NA: OFISI YA KATIBU MTENDAJI BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) 8 JUNI, 2018