SERIKALI imefunga vyuo vikuu 58 ambavyo vimekuwa vikihudumu kiharamu na kutoa digrii feki.
Tume ya kusimamia vyuo vikuu (NUC) ambayo huidhinisha taasisi za elimu ya juu, ilisema vyuo hivyo vimekiuka kanuni na sheria. Vyuo vikuu vilivyo na makao makuu yake nje ya Nigeria havitaruhusiwa kuhudumu nchini humo. Tume ya NUC ilionya wanafunzi waliohitimu kutoka vyuo vilivyofungwa hawatapata ajira katika idara ya serikali wala kuruhusiwa kuhudumu katika Shirika la Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYSC). Miongoni mwa vyuo vikuu vilivyofungwa ni chuo kikuu cha Royal, Atlanta, United Nigeria, London External Studies, Missouri USA kati ya vinginevyo.