-->

Mhadhiri wa chuo kikuu (muce) aliyemkashifu raisi mtandaoni akamatwa

idadi ya watu wanaokamatwa kwa tuhuma za kumkashifu raisi john magufuli kupitia mitandao ya kijamii zaongezeka baada ya police kumkamata mhadhiri wa chuo kikuu cha mkwawa Dr Oscar magava(48) Dr magava amekjwa mtu wa kumi kukamatwa na police katika kampeni ya jeshi hilo kwaajili ya kudhibiti uhalifu chini ya sheria ya uhalifu mtandaoni kamanda wa police mkoa wa iringa julius mjengialisema dr mgava alikamatwa akiwa sumbawanga na alirudishwa mkoani iringa mjengi alisema septemba 15 mwaka huu walipata taarifa kuwa mhadhiri huyo anatumia mitandao ya kijamii kumkashifu raisi mjengi aliendelea kusema waliamua kumsaka dr magava na walipopata taarifa kuwa dr magava amekwenda sumbawanga waliwasiliana na polisi wa huko wakamkamata na kumrudisha iringa hata hivyo kamanda mjengi hakuyataja maneno aliyotumia dr magava kumkashifu raisi kwa madai kuwa bado wanaendelea na uchunguzi na kwamba ukikamilika atafikishwa mahakamani kamanda mjengi aliwatahadharisha wananchi kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii wanatakiwa kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya maendeleo na sio kukashifu viongozi au watu wengine watu mbalimbali wamekuwa wakikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa hilo hilo

Read also-: