Roma aipigia magoti BASATA “mtaniua njaa jamani!”
Msanii
wa muziki wa hip hop, Roma Mkatoliki amefunguka kwa mara ya kwanza
ikiwa ni mwezi mmoja toka afungiwe na Baraza la Sanaa la Taifa
kujihusisha na shughuli za sanaa kutokana na kudaiwa kutoa wimbo
‘Kibamia’ ambao hauna maadili.

Basata wamesema walimfungia msanii huyo baada ya kutakiwa na baraza hilo
kubadili wimbo huo lakini hakufanya hivyo na kila alivyoita hakuweza
kutokea.
Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatato hii, Roma akiwa
na mwanae, Ivan amesema anawaomba BASATA kumpungia adhabu kwani hali
yake ya kiuchumi siyo nzuri.
“Haya yote yanaongeleka, lengo ni Roma aendelee kufanya muziki wake kwa
sababu muziki unamsaidia kama ajira, nyuma ya Roma kuna watu ambao
anawasaidia. Kwahiyo wakati mwingine naomba ieleweke kwamba tufanye tu
Roma aendelee na muziki wake ili maisha yake yaendelee,” alisema Roma.
Aliongeza,”Tena nikitoka hapa nitawasiliana na Katibu mkuu wa Basata
najua atanisikiliza, pia nimesikia Jumatatu kuna mkutano wa wasanii wote
na BASATA utafanyikia pale BASATA, zote ni katika njia ya kwenda
kuyaongelea haya mambo, lengo tuwe chombo kimoja,
Akiwa katika mahojiano hayo na mtoto wake, Ivan aliulizwa na matangazaji
wakipindi hicho kwanini hakwenda shule, na mtoto alisema hajaenda shule
kutokana na tatizo la ada.
“Sijakwenda shule leo baba hana ada,” alisema Ivan mb