-->

ushauri kwa wahitimu wa kidato cha nne 2018 baada ya kupokea matokeo nini cha kufanya

MAWASILIANO ZAIDI CONTACT 0754576387

*** Bofya hapa kunitumia text WhatsApp bila kusave number yangu**
WAkazi wa dar es salaam wanaweza kututafuta kwenye tuition centre yetu mpya iliyopo chamazi kwa ajili ya kuwafunza waalimu wa combination zote wapo


form five selection 2018/2019 tanzania bara bofya hapa








→→→→→SOMA LIST YA VYUO VINAVYOTAMBULIWA NA NACTE KWA KUBOFYA MAANDISHI MEKUNDU



  Kuna wadogo zetu wamepata matokeo yao ya kidato cha nne . Ni  muhimu sana kwenye maisha yao, kwa sababu ndio nguzo inayotoa upepo awe nani baadae kitaaluma kwa uchaguzi anaofanya sasa japo kwa baadhi wanaweza kuwa na wigo mpana wa kuchagua tena baadae.

kuna wengi ambao walipita huko na wana uzoefu wa matokeo tofauti, iwe ya kufaulu, wastani au kufeli na jinsi gani walijikwamua kutoka kwenye hali yaliyokuwa nao wakati husika.

  naamin blogteam tunaweza kuwapa mwanga hawa wadogo zetu wapunguze idadi ya makosa yanayotokana na kutokuwa na ufahamu ama kukata tamaa kwa kupata matokeo hafifu.


 Kwanza nawapongeza sana wadogo zangu kwa hatua waliyoifikia katika maisha yao Sio siri nikumbukumbu katika maisha. Kwa waliofaulu jiandaeni sasa mnarudi tena shule kuendelea na ngwe nyingine Hakikisha mapema sana umeshajua advance utaenda kusoma combination gani maana kule kupanikishana kupo na mwishowe .mkaona mambo magumu kumbe sio
Kufaulu ama kufeli yote ni mipango ya Mungu kikubwa tu nikutokufa moyo

       ushauri kwa waliosoma masomo ya science

Kama umesoma biology(B), physics(P), mathematics(M), chemistry(C), agriculture(A), food nutrion(N) na minor sana geography(G) hii inakuhusu

mhitimu kama umepata uwezo wa kufaulu masomo manne ya science hapo juu kuanzia grade (C) tafadhali hakikisha unasoma tahasusi za science advance bila kujali umefaulu masomo ya arts zaidi, mdau hii itakusaidia kucompete kwenye ajira pia utakuwa marketable pale umalizapo elimu yako ya advance na chuo.

wanafunzi wengi wamekuwa wakiogopa masomo ya science kutokana na kutishana wenyewe kwa wenyewe au kupokea ushauri mbovu kwa wahitimu waliotangulia na kufeli mitihani yao hivyo fikra hizi zimejengwa katika mioyo ya wanafunzi hadi leo.

Napenda kuwahimiza wahitimu watumie msemo huu (HATUSHINDWI) na wachukue uamuzi sahihi
       MUHIMU
Kama umefaulu physics hakikisha somo hilo unalihusisha katika tahasusi yako advance unashauriwa kupriotize tahasusi kama nitakavyo zipanga hapa kwa namba tahasusi ya kwanza ndio nzuri zaidi na zinazofuata zinazidi kuwa hafifu
1.PCB
2.PCM
3.PGM
4.CBA
5.CBN
6.CBG    
PCB ni tahasusi nyeti mno kwakuwa unaweza kuchagua degree programme nyingi sana wakati utakapo kuja kuomba chuo na pia ni marketable sana

PCM degree programme zake hazina compitition kubwa sana kwani ukikizi vigezo vya chini wakati unaomba chuo utapata chuo pia ni marketable sana na ukipata chuo lazima upate mkopo mdau naongezea na hii kama umesoma PCM nafasi ya kujiajiri ni kubwa mno


PGM tahasusi hii ni kama PCM ni marketable kiasi lakini sio kama PCM na PCB hii kutokana na kuwa na wanageographia wengi ila niwaondoe ukakasi kwa wale wasiojua pgm unaweza kusoma programme zote za engineering ufikapo chuo kama ilivyo PCM kwani wakati wa uchaguzi wako wataangalia ufaulu (phy na maths)

CBA tahasusi hii ni muhimu sana na ni marketable kwa waliosoma chemistry na hawakusoma physics tahasusi hii ni priority sana kwa wanafuzi wote waliosoma science lakini hawaakusoma physics pia imepewa kipaumbele chuo kikuu cha sokoine compition ni kubwa kiasi wakati wa kuomba nafasi chuoni hii inatokana na kukizana na wahitimu waliosoma PCB

CBN tahasusi hii ni muhimu compition ni kubwa kutoka kwa CBA na PCB ila ukisoma utaruhusiwa kusoma degree programme moja ya afya inayojulikana kama bachelor of science in mental health lakini waliosoma CBG na CBA hawana hiyo nafasi

CBG tahasusi hii ni marketable pia inakupa nafasi chache ya kuchagua degree programme compition ni kubwa mno kutoka kwa PCB, CBA, na CBN

ushauri kwa waliosoma masomo ya biashara

1. EGM
2. ECA
3. HGE
EGM mtu aliyesoma egm ana advantage ya kusoma programs kama IT,statistics,actuarial science,geology, computer science,building economics,architecture engineering,surveying nk hivyo anasoko kubwa kuliko wa HGE na pia anashindana sana na watu wa ECA yaan usoko wa ECA na EGM upo sawa but EGM degree programme zake ni nyingi na nzuri

HGE ni nzuri sana haswa inawabeba watu waliosoma masomo ya sanaa ili waweze kusoma masomo ya biashara na kujikimu kwa kuwa masomo ya sanaa sasa hayana soko kama yalivyo masomo ya biashara

 kama umesoma masomo ya sanaa

1. HGE
2. HGL
3. HGK
4. HKL
MUHIMU 
masomo ya sanaa hayana soko kubwa sasa lakini kwa waliosoma masomo ya sanaa wakahusisha language bado kuna uhitaji mkubwa wa watu kwenye ajira hivyo hakikisha kama umefaulu english soma HGL labda kama geography haujafaulu soma HKL ila kiswahili na history hamna soko

kama ulifeli english na umefaulu geography tafadhali soma HGE sikushauri sana kusoma HGK kwakuwa sio marketable kwa sasa

 kama huna sifa ya kujiunga na kidato cha tano shule za serikali tafadhali chagua shule binafsi au tafuta vyuo vya certificate

  BOFYA HAPA KUPATA SHULE ZOTE ZA PRIVATE NA GOVERMENT PAMOJA NA MAWASILIANO YA {UONGOZI WA SHULE AU WAHUSIKA JIRANI}

 

BOFYA HAPA KUPATA MAJINA YA VYUO NA SEHEMU VILIPO PAMOJA NA COURSE ZAKE 


kama huna sifa ya kujiunga na kidato cha tano na ungetamani kujiunga soma ushauri ila inabidi uwe sirious ili usipoteze muda na kupata hasara kubwa hii ni kwa wanaotafuta credit moja au mbili

Kupata shule ya kuanza kusoma form 5 ni suala dogo,Shule nyingi utakazoomba ujiunge na form 5 utapata,ila watakuuliza una plani gani ya kuziba hilo pengo la credit moja ili aweze kukubaliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita.
Kwa kuokoa mda watu wengi huwa WANAJITOA SADAKA,yaani unaanza kidato cha tano huku umejiandikisha kujiandaa kurudia mtihani wa kidato cha nne,ukifaulu na kupata hiyo "credit" ktk huo mtihani wa kidato cha nne uliourudia basi ni SALAMA yake,maana kikifika kipindi cha kujaza fomu za kuomba kufanya mtihani wa kidato cha sita utakubaliwa na utazijaza na zitapitishwa na BARAZA LA MITIHANI (NECTA).Ila kama ukifeli na kutopata hiyo credit moja ktk huo mtihani wa kidato cha nne uliourudia,hapo HATOKUBALIWA KUJAZA FOMU ZA KUOMBA KUJIANDIKISHA KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA,.na ikitokea wamejaza ki MAGUMASHI hapo shuleni kwako,basi kule Baraza la mtihani watagundua na hawatamkubalia ombi lako,HAWATAKUPATIA NAMBA YA KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA.Pia uwezekano wa kupata kesi ya ulaghai yaweza kukuandama.
Ila mara nyingi wanaojiandaa kurudia mtihani wa kidato cha nne ili kuzisaka credit zilizopungua huku wakisoma kidato cha tano huwa wanafaulu na kuzipata hizo credit kuliko kujiandaa wakati uko nyumbani.


 HAKIKISHA UNADOWNLOAD APP HAPO CHINI ILI  KUPATA NOTES, SYLABUS N.K KWENYE SIMU YAKO AU COMPUTER YAKO

1. Notes, Practicals na Review Question zaidi ya 20,000 Form I - VI Masomo yote
2. Masomo yote ya shule za Msingi, mazoezi na majaribio
3. Scholarships 4. Makala za Biashara
5. Makala za Jamii za kuondoa Msongo wa Mawazo

How to install in COMPUTER> click here

Read also-: