Watumishi 91 Wafukuzwa Kazi Serikalini
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amemwagiza katibu Mkuu wa Wizara hiyo
anayeshughulikia uvuvi Dk. Yohana Budeba pamoja na wakurugenzi wote wa
halmashauri za wilaya katika mikoa ya kanda ya ziwa................
Kuwafuta
kazi mara moja watumishi 65 na viongozi wa kamati za usimamizi wa
raslimali za uvuvi (BMU) 26 baada ya kubainika wanashiriki kufadhili
uvuvi haramu ndani ya ziwa Victoria.
Akihitimisha
operesheni maalum ya kitaifa ya kupambana na kudhibiti uvuvi na
biasahara haramu ya mazao ya uvuvi katika ukanda wa Ziwa Victoria
iliyodumu kwa siku 40, katika ukumbi wa chuo cha benki kuu jijini
Mwanza, Mpina amesema operesheni hiyo itaendelea hadi disemba mwaka huu
ili kuhakikisha uvuvi haramu unatokomezwa huku akidai hatasita
kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayebainika kukwamisha
juhudi za serikali.
Waziri
Mpina pia ameonesha kuchukuzwa na kitendo cha askari wa wanyamapori wa
hifadhi ya kisiwa cha Lubodo mkoani geita kuwazuia watendaji wa kikosi
cha operesheni hiyo wakati wa msako dhidi ya uvuvi haramu.
Operesheni
hiyo ilianza Januari mosi mwaka huu, ambapo jumla ya wadau 1,200
waliopo kwenye sekta ya uvuvi nchini walikutwa na makosa mbalimbali na
kutozwa faini ya shilingi Bilioni 4.7, huku tani 73 za samaki wasiokidhi
kiwango wakigawiwa kwa wananchi,na tani 173 za mazao ya uvuvi
zilitaifishwa,huku mali na zana mbalimbali za uvuvi zenye thamani kubwa
ya fedha zikiteketezwa kwa moto.