-->

Wakazi wa kisiwa cha Kojani Pemba wahamasika kuchimba vyoo na kuvitumia baada ya kupatiwa elimu ya afya na usafi wa mazingira.

Seebait.com 2017
SeeBait


kojaniNa Masanja Mabula -PEMBA
WAKAAZI wa kisiwa cha kojani wamesema  juhudi zinazofanywa na serikali pamoja na taasisi mbali mbali juu ya kuwaelimisha umuhimu wa matumizi ya vyoo  zimeleta mafanikio ambapo kwa sasa wamehamasika kuchimba vyoo na kuvitumia.
Wamesema kabla ya kuelimishwa umuhimu wa kutumia vyoo, walikuwa wakitumia sehemu za fukwe za bahari kwenda haja kubwa na ndogo, hali ambayo ikiweza kusababisha maradhi ya miripuko wakati wa mvua zinaponyesha.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, walisema kuwa  kwa sasa hali ni tofauti na zamani ambapo wananchi wameelimika na wanatambua umuhimu wa kutumia vyoo .
“Kwa kweli ilikuwa hatujui lolote kuhusu utumiaji wa vyoo, kwani likuwa tunajisaidia kwenye mikandaa, lakini kwa sasa hatutaki tena kujisaidia sehemu zisizostahiki.
Nae sheha wa shehia ya Mpambani Kojani Ali Omar Ali  alieleza kuwa, hali ya matumizi ya vyoo kwa sasa inaridhisha kutokana na Serikali kuwaelimisha wananchi kutambua matumizi sahihi ya vyoo .
“Juhudi zilizofanywa na serikali na taasisi zimezaa matunda, kwani wananchi kwa kiasi kikubwa wamechimba vyoo na wanavitumia, kwa kweli ni faraja kwetu”, alisema sheha huyo.
Kwa upande wake  mwakilishi wa Jimbo la Kojani  Makame  Said Juma alisema,  baada ya kuelimishana na kuona umihumu wa vyoo, wananchi wa kojani wanaendelea na ujenzi wa vyoo na kusema iko haja kuongeza nguvu na hamasa ili hali iende vizuri zaidi.
“Vyoo ni muhimu kwetu, hivyo nawaomba wananchi wa kisiwa hicho kuzidisha nguvu ya kuchimba vyoo, ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza”, alieleza mwakilishi huyo.
Wananchi wa kisiwa cha Kojani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, walikuwa wakikabiliwa na tatizo la kutokuwa na vyoo, ambapo kwa sasa wamehamasikakuchimba na kuvitumia.

Read also-: