-->

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO VYA HABARI



CrcmP1xWIAIjnXD
WATU WAWILI WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE 26 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA MVUA YENYE UPEPO MKALI ULIOEZUA PAA LA KANISA WAKATI WAKENDELEA NA IBADA WIALAYANI MAGU.

KWAMBA TAREHE 19.02.2017 MAJIRA YA SAA 15:30HRS KATIKA KIJIJI NA KATA YA LUBUNGU TARAFA YA ITUMBILI WILAYA YA MAGU JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. NGWAKU NKULUMBI MIAKA 55, MWANAMKE NA MKAZI WA KIJIJI LUBUGU, NA 2. MIGAYI HERENICO, MIAKA 12, MTOTO WA KIKE NA MKAZI WA KIJIJI CHA LUBUGU, WALIFARIKI DUNI KATIKA AJALI YA MVUA ILIYOKUWA NA UPEPO MKALI ILIYOEZUA PAA LA KANISA LA DHEHEBU LA ROMANI KATHOLIKI WAKATI WAUMINI WA KANISA HILO WAKIENDELEA NA IBADA NA KUJERUHI WAUMINI WENGINE 26, KATI YA HAO MAJERUHI 07 HALI ZAO BADO SIO NZURI WAMEPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA MATIBABU ZAIDI HUKU MAJERUHI 17 WAKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MAGU NA MAJERUHI 02 TAYARI WAMERUHUSIWA.

INASEMEKANA KUWA IBADA YA TAREHE TAJWA HAPO JUU ILIKUWA IMEHUDHURIWA NA ZAIDI YA WAUMINI MIA MOJA , LAKINI ILICHELEWA KUANZA KWA SABABU PADRE WA KANISA HILO AITWAYE MICHAEL KUMALIJA MIAKA 60 AMBAYE  ALIKUA AMEANZA KUHUDUMIA KATIKA KANISA LA JIRANI NDIPO ILIPOFIKA MAJIRA TAJWA  HAPO JUU PADRE ALIFIKA NA KUANZA KUENDESHA IBADA. AIDHA INASEMEKANA KUWA WAKATI IBADA IMEANZA KUTOLEWA ILIANZA KUNYESHA  MVUA YENYE UPEPO MKALI AMBAYO ILIEZUA PAA LA KANISA HILO.

AIDHA INADAIWA KUWA BAADA YA TUKIO HILO KUTOKEA WAUMINI WALIANZA KUKIMBIA KUTOKA NJE YA KANISA HUKU KILA MMOJA AKIJARIBU KUNUSURU MAISHA YAKE, NDIPO BAADA YA TUKIO HILO KUPITA ILIGUNDULIKA KUWA WATU WAWILI WAMEFARIKI DUNIA NA KUJERUHI WENGINE 26, AMBAPO MAJERUHI 7 AMBAO MAJINA YAO BADO HAYAJAFAHAMIKA WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA MATIBABU ZAIDI, HUKU WENGINE 17 WAKIENDELEA NA MATIBABU HOSPITALI YA WILAYA YA MAGU NA MAJERUHI 02 WAKIWA TAYARI WAMERUHUSIWA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO SENGA ANATOA POLE KWA WAUMINI WOTE WA KANISA KATOLIKI WILAYA YA MAGU KWA MAAFA  YALIYOWAPATA, AIDHA ANAWASHAURI WAKAZI WOTE WA JIJI NA MKOA WA MWANZAKUBORESHA MAKAZI NA NYUMBA ZA IBADA ILI KUWEZA KUKABILIANA NA MAAFA YA AINA KAMA HII PINDI YANAPOTOKEA.

IMETOLEWA NA;

ACP: AUGUSTINO SENGA

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA

Read also-: