NAIBU WAZIRI NISHATI NA MADINI ATEMBELEA KITUO CHA KUFUA UMEME CHA NYAKATO JIJINI MWANZA
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akielezwa jambo na Meneja wa Kituo cha Kufua umeme kwa kutumia mafuta mazito (HFO) cha Megawati 60 cha Nyakato Jijini Mwanza, Mhandisi Mathew Mwangomba (kushoto). Kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi John Mageni.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kulia) akikagua Kituo cha Kufua umeme kwa kutumia mafuta mazito (HFO) cha Megawati 60 cha Nyakato Jijini Mwanza. Kushoto ni Meneja wa kituo hicho, Mhandisi Mathew Mwangomba.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akielekeza jambo wakati wa ziara ya kukagua mitambo ya kuzalisha umeme ya Nyakato Jijini Mwanza. Kulia ni Meneja wa Mitambo, Mhandisi Mathew Mwangomba.
Moja ya mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta mazito (HFO) kwenye Kituo cha kufua umeme cha Nyakato jijini Mwanza. Kituo hicho kina jumla ya mitambo 10 yenye uwezo wa kuzalisha kiasi cha Megawati 60 huku kila mtambo ukiwa na uwezo wa kuzalisha kiasi cha Megawati sita.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akikagua moja ya mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta mazito kwenye kituo cha Nyakato jijini Mwanza
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kulia) akimsikiliza Meneja wa Mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta mazito (HFO) ya Nyakato Jijini Mwanza, Mhandisi Mathew Mwangomba alipofanya ziara ya kukagua mitambo hiyo ili kujionea utendaji wake.