-->

POLICE TANZANIA WAUWA JAMBAZI KABLA YA KULIPUA BOMU


SATURDAY, OCTOBER 8, 2016

Polisi waua jambazi kabla hajalipua bomu








Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba  
By Burhani Yakub, Mwananchi byakub@mwananchi.co.tz
Lushoto. Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi, huku mmoja akiwahiwa kabla hajalipua bomu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amesema tukio la kwanza lilitokea Jumanne saa nne na nusu asubuhi, askari walipofanya operesheni ya kuwasaka majambazi katika Msitu wa Mafi.
Wakulyamba amesema mtu huyo aliyetambulika kwa jina moja la Omar, walimuua wakati akikimbia kutoka msituni alipokuwa amejificha.
Amesema mtuhumiwa alikuwa ameshika bomu mkononi, lakini askari walimuwahi kwa kumpiga risasi kabla hajalirusha na kusababisha madhara.
“Alikurupuka kutoka kwenye kichaka eneo la msitu huo... wakati akijiandaa kurusha bomu askari walimmiminia risasi,” amesema.
Katika tukio jingine lililotokea Jumatano, mkazi wa jijini Dar es Salaam,  Issa Anyingise (42) anayedaiwa kuwa ni jambazi aliuawa na polisi kwa kupigwa risasi.
Wakulyamba amesema tukio hilo lilitokea saa kumi na mbili jioni wakati mtuhumiwa huyo akijaribu kuwatoroka askari waliokuwa wakifanya msako nyumbani kwake.







Read also-: