WANAWAKE 13 WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 2 KWA KOSA LA KUJIUZA HUKO MOROGORO
Dada poa hao wakitoka ser
Dada poa huyu baada ya kutoanm kwenye sero na kumshuhudia Mwandishi wa habari hizi akiwapiga picha mahakani hapo alificha sura yake.
Warembo hao baada ya kukamtwa jumatano iliyopita usiku mnene wakiwa wamevaa vinguo vya vya mitege'Vimini' siku iliyofuta ndugu zao waliwaletea nguo za heshima na kutinga nazo mahakamani kama wanavyooneka pichani.
Ukiwa kwenye windo ukivaa mavazi haya utampata nani?
Difenda hilo likiwapeleka Magereza wakaanze maisha Mapya huku baadhi ya ndugu zao wakiwashuhudia
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
ILI Kuonyesha serikali ya sasa hailazi damu na kwamba moto unawaka kila kona ili Mambo yaende sawa na kwa spidi kubwa warembo wapatao 13 wamejikuta wakihukumiwa kwenda jela miaka miwili[2] kila mmoja baada ya kukiri kosa lao mbele ya Mahakama.
Katika sakata hilo lililoshuhudia na Mwandishi wa habari hizi mwiashoni mwa wiki iliyopita warembo hao walipigwa mvua hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha na biashara haramu ya kuuza mwili na kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzi ya Nunge Mkoani hapa.
Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo wanawake hao walikamatwa na Polisi usiku mnene wakiuza Miili yao kwenye kambi korofi ya Ufuska ya ltigi iliyopo Msamvu Kata ya Mwembesongo Mjini hapa ambapo walifunguliwa kesi namba 155 ya mwaka 2017.
Hukumu hiyo ilitolewa na hakimu ya Mahakama hiyo Emelia Halosi Mwambagi baada ya watuhumiwa hao kukiri kosa mbele ya Mahakama hiyo wakidai walifanya hivyo kutokana na ugumu wa Maisha.
Hata hivyo hakimu huyo alisema aliwahukumu warembo hao kwenda jela miaka 2 kila mmoja kwa kosa la uzururaji na kujiuza na kujipatia kipata kwa kuuza mwili ili iwe fundisho kwa wanawake wengine wanaofanya biashara hiyo haramu.

Akizungumza na Mtandao huu katika Mahojiano Maalumu baada ya hukumu hiyo,hakimu huyo alikuwa na haya ya kusema.
"Kuna biashara nyingi za kufanya kama vile Mama Ntilie na Vibarua vya kulima. kuuza mwili ni kujidharirisha na kudharirisha wanawake wengine nimetoa hukumu hii ili tahadhari kwa wengine wanaofanya hivyo"alisema
Baada ya kusomewa hukumu hiyo warembo hao walijikuta wakipigwa na butwaa huku wakishidndwa kuamini kilichotokea kwani walidhani wangepigwa faini ya kiasi kidogo cha fedha kisha kurejea uraiani lakini ndio kwanza maafande kupanda Difenda kuelekea Gerezani kuanza kutumikia adhabu hiyo.