TAHLISO Yatoa Tamko Kuhusu Wanafunzi Wanaotaka Mwigulu Ajiuzulu Kwa Kifo Cha Akwilina
TAARIFA KWA UMMA
Ndugu waandishi wahabari tunawashukuru sana kwa kukubali wito wetu wakuja kujumuika pamoja nasisi.
Leo tarehe 3/3/2018 tumekutana na viongozi wa vyuo vikuu nchi nzima kwa ajili yakujadili changamoto zinazotukabili.
Kikao hiki ni cha TAHLISO Baraza Kuu (SENATE) kina husisha Maraisi wa serikali za wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini.
Tunatambua
kwamba kuna kifo cha mwanafunzi mwenzetu Akwilina Akwilini,mwanafunzi
wa chuo cha NIT kilichotokea mwezi wa pili. Tunawashukuru wanafunzi
wenzetu kwa utulivu mkubwa na mshikamano waliouonesha tangu msiba
ulipotokea, wakati wa kipindi cha majonzi hadi kufikia sasa.
Tunamshukuru
Mhe.Raisi wa Jamuhuri ya Muunganowa Tanzania kwa kuingilia kati suala
hili na kuagiza uchunguzi ufanyike na hatua za kisheria zichukuliwe kwa
wote watakaobainika kuhusika na kifo cha Akwilina Akwilini.
Vilevile tunaishukuru Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ukaribu waliouonesha katika kipindi chote cha msiba.
Tunaomba wanafunzi waendelee kuwa watulivu wakati maagizo ya Mh. Raisi yakitekelezwa.
Aidha
tunapenda jamiii tambue kuwa TAHLISO ndio chombo kikuu cha kuwasemea
wanafunzi wote nchi nzima Tanzania na sio kikundi kingine chochote
kile.
Vipo
vikundi vingi vimejitokeza na kutoa matamko mbalimbali baada ya kifo
hiki kutokea, vikundi vingine vikaenda mbali Zaidi kwakuwataka baadhiya
watendaji wa Serikali akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani kujiuzulu jambo
ambalo linaashiria vikundi hivyo kuongozwa ama kutumika na makundi ya
kisiasa, haiwezekani kutaka watendaji wa Serikali wajiuzulu wakati
uchunguzi bado unafanyika na matokeo ya uchunguzi huo bado hayajatoka.
Jambo
la kusikitisha Zaidi kuna baadhi ya vikundi vimejitangaza kwamba
vinaungwa mkono na Maraisi wa Vyuo Vikuu jambo ambalo sio la kweli,
Marais wote wa Vyuo Vikuu tuko hapa Dodoma tunaendelea na vikao vyetu
vya kujadili changamoto zinazowakabili wanafunziwa Vyuo Vikuu.
Tunatoa
wito kwa vikundi vyote vinavyojihusisha nakutumia mwamvuliwa Marais wa
Vyuo Vikuu kama kinga yao ili kuu hadaa Umma kwamba wanaungwa Mkono,
vikundi hivyo viache tabia hiyo vinginevyo tutawachukulia hatua za
kinidhamu.
TAHLISO
tunasubiri matokeo ya Uchunguzi unaofanyika juu ya kifo cha Akwilina na
tunaimani wahusika wote watachukuliwa hatua kali zakisheria.
Tunawaomba
wanafunzi wote tuendelee kuwa watulivu wakati tukisubiri matokeo hayo
na kujiepusha na maandamano na vitendo vyovyote vitakavyo sababisha
uvunjifu wa Amani nakuleta mgawanyo miongoni mwa wanafunzi.
Hata
hivyo namna bora yakufikisha hoja nikutumia njia ya majadiliano kama
wasomi badala ya kutumia nguvu ama maandamano kwakutofuata taratibu na
madhara yake ni kusababisha vuruguzi sizotakiwa na hatimaye kuhatarisha
usalama na hivyo kuathiri jamii kwaujumla wake.
Vurugu
zozote zitokanazo kwakutozingatia taratibu zinaweza kudhorotesha
shughuli za kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na Uchumiwa Taifa letu.
Vile
vile zinapoteza mvuto kwawawekezaji wanje na wandani, ikiwemo shughuli
za utalii nchini ambazo zinachangia pato la Taifa letu.
Athari
za Vurugu na kukosekana kwa amani zipo wazi natunaziona kwa nchi
nyingine zikiwemo baadhi ya nchi jirani zetu ambao wamekua wakimbizi
nchini kwetu kila siku.
Tunaona
kuwa kama wanataaluma tunajukumu kubwa la kuelimisha jamii na kuwamfano
bora wakutumia njia za majadiliano katika kujenga hoja zetu
ilizitatuliwe kuliko kutumia njia ya maandamano au vurugu zisizo na
ulazimawowote.
Taasisi hii ndio yenye dhamana ya kutetea nakusimamia maslahi ya wanafunzi wote wa vyuo na vyuovikuu Tanzania na si vinginevyo.
………………………………….
GEORGE ALBERT MNALI
MWENYEKITI
TAHLISO