Naibu Waziri Ole Nasha: Sijaridhishwa na ukarabati uliofanyika Butimba
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa William Ole Nasha ameitaka Wizara yake
kufanya uchunguzi na kutoa ripoti ya namna ukarabati wa Miundombinu
ulivyofanyika katika Chuo cha Ualimu Butimba ili kujiridhisha kama kweli
ukarabati huo unaakisi kiasi cha fedha zilizotolewa.
Naibu
Waziri Ole Nasha ametoa kauli hiyo Mjini Mwanza baada ya kufanya ziara
katika chuo hicho hapo ambapo amesema hajaridhishwa na ukarabati
ulivyofanyika kwa kuwa Chuo hicho kilipatiwa kiasi cha
takribani Milioni Mia Nane Sitini na Tatu.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akikagua
moja ya Bweni la Wanafunzi katika Chuo cha Ualimu Butimba lililofanyiwa
ukarabati na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Programu ya
Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R).
Ole
Nasha amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha Vyuo vya Ualimu
vinakuwa na mazingira mazuri ya kuwaandaa Walimu wanaokwenda kufundisha
katika shule mbalimbali hapa nchini hivyo ni jukumu la Wakuu wa
Taasisi na Vyuo vya Elimu kuhakikisha wanasimaia Miradi mbalimbali ya
Elimu kwa ukamilifu na kuwa Serikali haitasita kuchua hatua kwa yeyote
atakayeshindwa kusimamia Miradi hiyo kwa weledi.
“Chuo
hiki kimepatiwa takribani Milioni Mia Nane Sitini na Tatu kwa ajili ya
ukarabati wa miundombinu kama hivi ndivyo ukarabati uliofanyika
hauonyeshi thamani ya fedha iliyotolewa kwa ajili ya Chuo hiki cha
Ualimu Butimba, kwa kweli Sijaridhishwa”alisisitiza Naibu Waziri huyo.
Akitoa
maelezo Mkuu wa Chuo hicho John Ole Meiludie amejitetea kuwa kazi hiyo
ya ukarabati imefanyika kwa umakini isipokuwa wanafunzi wenyewe ndiyo
wanachana nyavu za madirisha lakini pia hali ya mvua zinaponyesha
huondoa rangi ambayo inakuwa imepakwa katika majengo ya Chuo hicho.
1. Naibu Waziri wa Elimu akipokea maelezo katika maabara ya baiolojia Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole akipokea
maelezo kutoka kwa Mkufunzi Ramadhani Wenge kuhusiana na maabara ya
Bailojia iliyopo katika Chuo cha Ualimu Butimba Mkoani Mwanza.
Akiwa
Mkoani Mwanza Naibu Waziri Ole Nasha ametembelea Shule ya Sekondari
Nyegezi iliyoko Wilaya ya Nyamagana na Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma
VETA kilichopo wilaya ya Ilemela na kuridhishwa na namna walivyotekeleza
miradi ya Elimu.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akiongea
na Wanafunzi wa Shule ya sekondari Nyegezi Iliyopo Mkoani Mwanza
alipofanya ziara shuleni hapo kukagua miradi inayotekelezwa na Programu
ya Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R).