-->

MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA KUMBUKUMBU YA SEBASTIAN KOLOWA - SEKOMU (ZAMANI SEKUCO) KILICHOPO LUSHOTO - TANGA, ANAKARIBISHA MAOMBI YA KUJIUNGA NA CHUO MWEZI APRIL, 2018 KWA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA KATIKA FANI ZIFUATAZO:



KOZI ZA STASHAHADA (DIPLOMA)
  1. Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi (Ordinary Diploma in Primary Education)
 Muda: Miaka Miwili.
  Sifa za kujiunga:
  1. Alama za Ufaulu ni D NNE (4) katika Kidato cha Nne NA Cheti cha Ualimu wa daraja IIIA
  2. Ufaulu katika kidato cha Nne daraja la I-III au G.P.A 1.6 au Zaidi  NA Cheti cha Msingi cha Ngazi ya Nne (NTA Level 4) cha Ualimu  kilichotolewa na NACTE au Mamlaka nyingine inayotambuliwa (isiwe chini ya mwaka mmoja)
  1. Stashahada ya Sheria (Diploma in Law)
 Muda: Miaka Miwili.
 Mahali: Kituo cha Tanga na Lushoto
               Sifa za kujiunga:
  1. Kidato cha sita ufaulu alama moja na Subsidiary/Unsatsifatory moja na angalau alama nne za ufaulu katika kidato cha nne.Mwombaji lazima awe amefaulu Kiingereza katika kidato cha nne. AU;
  2. Astashahada ya Sheria kutoka vyuo au taasisi zinazotambuliwa na NACTE.
  1. Stashahada ya Uongozi wa Biashara (Diploma in Business Administration)
  Muda:   Miaka Miwili.
 Mahali: Kituo cha Tanga na Lushoto.
            Sifa za kujiunga:
  1. Alama MOJA (1) ya ufaulu au zaidi ya kidato cha sita katika masomo ya Hesabu, Biashara au Uhasibu. Tofauti na masomo haya lazima mwombaji awe amefaulu Hesabu au Biashara au Book keeping Kidato cha nne AU;
  2. Astashahada ya Uongozi wa Biashara iliyotolewa na chuo kinachotambulika na NACTE.
  1. Stashahada ya Uhasibu na Fedha (Diploma in Accounting and Finance)
Muda: Miaka Miwili.
Mahali: Kituo cha Tanga na Lushoto.
        Sifa za kujiunga:
  1. Alama MOJA(1) ya ufaulu au zaidi ya kidato cha sita katika masomo ya Hesabu, Biashara au Uhasibu, tofauti na masomo haya lazima awe amefaulu Hesabu au Biashara au Book keeping Kidato cha nne AU;
  2. Astashahada ya Uhasibu na Fedha iliyotolewa na chuo kinachotambulika na NACTE.
  1. Stashahada ya TEHAMA (Ordinary Diploma (NTA Level 6) in Computing, Information and Communication Technology)                        
Muda: Miaka Miwili.
Mahali: Lushoto
Sifa za kujiunga:
  1. Cheti cha Msingi cha Ufundi (NTA  Level 4) katika ICT,CICT kinachotambuliwa na NACTE, AU;
  2. Alama ya ufaulu MOJA (1) na Subsidiary MOJA (1)  katika Kidato cha Sita NA
Ufaulu katika masomo ya Hesabu na Kiingereza katika kidato cha Nne.

KOZI ZA ASTASHAHADA (CERTIFICATE)
  1. Astashahada ya Sheria (Certificate in Law)
Muda: Mwaka Mmoja.
Mahali: Kituo cha Tanga na Lushoto.
  Sifa za kujiunga:
  1. Alama NNE (4) za ufaulu au zaidi, mojawapo ikiwa ni ya Somo la Kiingereza katika kidato cha nne, AU;;
  2. Kidato cha sita angalau alama moja ya ufaulu. Kama alama hiyo sio Kiingereza basi mwombaji awe amefaulu somo hilo katika kidato cha nne.
  1. Astashahada ya Uongozi wa Biashara (Basic Technician Certificate in Business Administration)
 Muda: Mwaka Mmoja.
 Mahali: Kituo cha Tanga na Lushoto.
               Sifa za kujiunga:
  1. Alama NNE (4) au zaidi za ufaulu kidato cha nne mojawapo likiwa somo la Hisabati au Biashara.
  1. Astashahada ya Uhasibu na Fedha (Basic Technician Certificate in Accounting and Finance)
 Muda: Mwaka Mmoja.
Mahali: Kituo cha Tanga na Lushoto.
          Sifa za kujiunga:
  1. Alama NNE (4) au zaidi za ufaulu kidato cha nne.
  1. Astashahada ya TEHAMA (Basic  Technician Certificate (NTA 4) in Computing, Information and Communication Technology)                                                           
Muda: Mwaka Mmoja
 Mahali: Kituo cha Tanga na Lushoto
         Sifa za kujiunga:
  1. Alama Nne za ufaulu kidato cha Nne.  Alama hizo zijumuishe pia Somo la Hesabu na Kiingereza. AU;
  2. Cheti cha National Vocational Award (NVA) Level II. AU; (Trade Test Grade II)   katika ICT kutoka Mamlaka inayotambuliwa, NA Cheti cha Kidato cha Nne

Kozi hizi zitaanza tarehe 23/04/2018

Kwa mwanafunzi atakayemaliza programu ya cheti na kufaulu vizuri atakuwa amepata sifa ya kujiunga na stashahada na baadaye shahada inayoendana na programu husika.

Mwisho wa kuwasilisha maombi ni Ijumaa tarehe 30/03/2018, saa 10 jioni

DOWNLOAD APPLICATION FORM               


Kwa msaada zaidi piga simu au tuma ujumbe mfupi kwenda namba zifuatazo: 0712811420 au: 0756555876

Read also-: