Taarifa Kwa Umma Kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako
amekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya Viongozi wa wamiliki wa
shule binafsi za sekondari ambapo kwa pamoja
wamejadili utekelezaji Wa waraka Namba. 7 unaokataza wanafunzi kufukuzwa
shule kwa sababu ya kutofikisha wastani wa ufaulu uliowekwa na shule.
Waziri Ndalichako ameeleza ameeleza kuwa chimbuko la waraka huo ni
baadhi ya shule kufukuza idadi kubwa ya wanafunzi wakiwa Mwaka wa mwisho
wa masomo yao kwa kigezo cha kutotimiza wastani unaotakiwa kitendo
ambacho amekielezea kuwa kuwa ni cha kibaguzi na ki-unyanyasaji.
" Mfano shule ya sekondari Pandahil ambayo imefukuza watoto 148, shule
ya sekondari star high imefukuza wanafunzi 49 hizo ni baadhi tu, Aidha,
ameeleza kuwa Wakati Bunge na Serikali ikisikitika pale Wasichana
wanapopata uja uzito na kuacha shule, Waja sekondari na Musindi
sekondari zimefukuza wanafunzi wa kike 15 kila moja kwa kigezo cha
ufaulu mdogo.
Waziri huyo amesisitiza kuwa wizara itaendelea kusimamia utekelezaji wa
waraka huo na amewataka Viongozi hao kuweka utaratibu mzuri kwa
wanafunzi walio na uwezo mdogo badala ya utaratibu uliopo sasa wa
kuwafukuza shule na hivyo kuwaacha wakiwa hawana pa kwenda.
Kwa upande wao viongozi wa wamiliki wa shule wameeleza kuwa utekelezaji
wa waraka huo utasababisha kushukuka kwa Ubora Wa ufaulu katika shule
zinazomilikiwa na watu binafsi.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt
Leonard Akwilapo kikao ambacho kimefanyika jijini Dar es salaam.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
22/01/2018