-->

MGAMBO ALIYEZUSHA KUFUFUKA KWA MFU MOCHWARI ATIWA MBARONI

dMgambo katika Hospitali ya Mkoa wa Singida, amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kuwa Rahel Erasto (28), aliyefariki dunia wiki iliyopita amefufuka na kuzua mtafaruku kwa ndugu na jamaa zake. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Mayala Towo alisema tukio la Rahel, aliyekuwa mkazi wa Minga Manispaa ya Singida kudaiwa kufufuka lilitokea Ijumaa iliyopita alasiri katika hospitali hiyo. Alisema Septemba 29, Rahel alifikishwa katika hospitali hiyo kujifungua. “Kutokana na sababu za kitabibu, alifanyiwa upasuaji na kutolewa mtoto wa kiume akiwa hai. Lakini kwa bahati mbaya alifariki dunia (Rahel) usiku wa Septemba 30,” alisema. Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Singida, Dk Ramadhan Kabala alithibitisha kuwapo kwa taarifa hizo na kudai kuwa mwili wa marehemu unaendelea kufanyiwa uchunguzi.

Read also-: