-->

HISTORIA YA SCORPION


Historia fupi ya Scorpion anayedaiwa kumngoa mtu Macho



Alivyokua mdogo alikataa kusoma mama yake alisha fariki siku nyingi na alikua akilelewa na mama yake mdogo maeneo ya Yombo Buza.

Alishawahi kufungwa jele japo bado haijafahamika kosa lilikua nini, na jinalake kamili ni Salum Njopwe na jina hili ni la babu yake. Yeye ni mwenyeji wa mkoa wa Shinyanga. Kwa mujibu wa mama ya mdogo anasema Scorpion alipokua akitoka nyumbani usiku saa mbili anamuaga mama yake mdogo kuwa anakwenda kwenye kazi ya ubaunsa katika club kumbe mwenzie alikua anaenda Buguruni kuibia watu paka asubuhi ndo anarudi.
Pia scorpion ashawahi kushiriki katika shindano lijulikanalo kama Dume Challenge kama miaka mitatu iliyopita na aliibuka mshindi. Napia alianza mafunzo ya kucheza karate tangu akiwa mdogo sana na pia ni mtu mwenye nguvu za kuzaliwa nazo.


Kuna kipindi aliondoka nyumbani kwao kwamuda mrefu mama yake mdogo anadai alikua hajui yuko wapi mpaka baadae aliporudi nyumbani mwenyewe.

Amekamatwa na polisi baada ya kutuhumiwa kumjeruhi mkazi mmoja wa Dar es salaam enele la Buguruni kwa kumngoa macho katika kitendo kilichoelezwa kuwa ni wizi wa fedha

Read also-: