-->

WANAFUNZI 28 WA UUGUZI WASIMAMISHWA MASOMO-MBEYA

  1. Wakieleza wanafunzi hao wanasema
    Tarehe 9/07/2018 walianza mithiani ya majaribio mock ambayo ilifanyika nyanda za juu kusini katika siku ya pili ya mithiani hiyo wasimamizi wa ndani (walimu wa chuo hicho) walisema mithiani hiyo ilivuja na hivyo kuchukua jukumu la kwenda nje ya chumba cha mthiani na kuchukua mikoba ya wanafunzi hao iliyokua na material waliyokua wanasoma wanafunzi pamoja na simu za mikononi ambapo wanafunzi hao waliiweka nje ya darasa..Baada ya hapo simu hizo ziliwashwa na walimu hao na kuanza kusoma message na kuangalia picha zilizopo katika kile ambacho wao walikiita ni upekuzi wa kugundua mithiani iliyovuja.Walimu hao walienda mbali zaidi na kwenda kukusanya simu zilizopo kwenye hostel za wanafunzi na kuendelea na upekuzi..Katika siku ya pili yaani tarehe 11/07/2018 mahojiano ya kumuhoji mtu mmoja mmoja kati ya ofisi ya chuo hicho kitengo cha uuguzi yaliendelea.Mahojiano hayo yalikua yakiendeshwa chini ya kaimu mkuu wa chuo ambapo wanafunzi walilazimishwa waseme kuwa walikutwa na majibu kwenye chumba cha mthiani na wakilazimishwa wataje walipotoa majibu hayo.
    Tarehe 12/07/2018 mahojiano yaliendelea ambapo inareportiwa kuwa mwanafunzi mmoja anayejiendeleza ambaye jina lake halikupatikana mara moja alifungiwa kwenye chumba cha chuo hicho kwa masaa zaidi ya 8 akiwa na mtoto wa mwezi mmoja na nusu, walimu wa chuo hicho walimuweka kizuizini ikiwa ni njia ya kumlazimisha aseme material yale alipoyapata.
    Katika hali ya kusikitisha inareportiwa kuwa kumekua na vitendo vikubwa vya udhalilishaji na uvunjaji wa haki za binadamu hasa kwa wale wanaoonekana kuwa ni wakereketwa au wapenzi wa Chama tawala (CCM)
    Hadi taarifa hizi zinaandikwa hakukua na uthibitisho wowote wa kuvuja kwa mithiani hiyo ,vyuo vyote vilivyoshiriki kufanya mithiani hiyo havijareport popote uvujaji wa mithiani hiyo na ata chuo husika (operating theatre management mbeya-(chuo cha rufaa))hakijareport uvujaji huo sehemu yoyote.
    Alipotafutwa kaimu mkuu wa chuo hicho kuzungumzia taarifa hizi simu yake haikupokelewa .
    Alipopigiwa kwa mara nyingine simu yake haikupatikana.

Read also-: