Utendaji Kazi Chuo Kikuu SUA Wamfurahisha Rais Magufuli.....Awashangaa Wanaosema Elimu ya Tanzania Imeshuka
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka
na kusema watu ambao wanasema elimu imeshuka nchini wanakosea kwani kuna
sehemu ambazo elimu inaonekana ipo vizuri akitolea mfano wa chuo cha
kilimo cha Sokoine University of Agriculture (SUA).
Magufuli
amesema hayo leo Mei 7, 2018 akiwa katika ziara yake mkoani Morogoro na
kusema kuwa watu wasiseme kwa ujumla kushuka kwa elimu ili hali kuna
sehemu watu wanafanya vizuri katika elimu, na kudai kuwa wa SUA wameweza
kufundisha mpaka Panya na akaelewa hivyo ni wazi kuwa wapo vizuri sana.
"Unajua
hata watu ambao wanasema elimu imeshuka sijui kama wamefika hapa kwa
sababu wangefika hapa na kumuona Panya anajua bomu liko wapi nadhani
asingesema elimu imeshuka, wanamuona Panya amefundishwa mpaka akaelewa
eti binadamu ndiyo asielewe, mjue walimu wa hapa wanafundisha mpaka
Panya siyo binadamu tu, mpaka anaelewa akinusa hapa kuna kifua kikuu"
Rais
Magufuli aliendelea kuzungumzia jambo hilo na kusema kuwa walimu wa SUA
na wanafunzi wapo vizuri sana katika masuala ya shule ndiyo maana
wanaweza kufanya gunduzi mbalimbali ambazo zinatija na msaada katika
maisha ya kila siku.
"Wanafundisha
Panya mpaka anatengeneza mapapai mpaka anafanya 'crossbreeding',
anafanya papai lianze kuzaa likiwa na miezi mitano badala ya kusubiri
miaka mitano halafu linazaa 'production' ya matunda mawili matatu, hizi
kazi wamefanya hawa watu yaani hapa kuna vichwa tuache 'generalization'
lakini pia lazima tuelewe elimu yetu imetoka wapi, palikuwa na elimu ya
UPE aliiacha baba wa taifa kwa sababu hapakuwepo watu wa kwenda
kufundisha"
"Nakumbuka
baadae likaja suala la kupeleka walimu nafikiri ilikuwa enzi za Mwinyi
au Mkapa mtu ukipata 'division zero' kidato cha nne au 'division four'
unapelekwa ualimu hayo ndiyo matokeo, tulifanya hivyo kwa sababu ya hali
halisi ya wakati huo, tumekuja kwenye awamu iliyopita mimi nimefukuza
wanafunzi karibu elfu saba pale UDOM yaani 'four four' wanakwenda
kuchukua 'Degree' walipelekwa kwenye awamu ya nne, kwa hiyo ukifuatilia
unaweza kujua tumetoka wapi na tunaelekea wapi" alisisitiza Rais
Magufuli
Mbali
na hilo Rais Magufuli amekiri kuwa katika awamu yake ya tano wamekuja
na elimu bure na kusema kuwa huenda baadae ikaja kuwa na madhara ila
itasaidia kuondoa ujinga kwa watu wengi ambao walikuwa wakikosa elimu
hiyo kwa sababu ya kukosa ada ya kulipa shule.
"Na
sisi tumekuja tumeingiza elimu ya karo bure wanafunzi wameongezeka
walioingia darasa la kwanza wameongezeka mara mbili zaidi wakawa milioni
mbili kutoka milioni moja, hivyo inawezekana hii nayo ikaleta madhara
baadaye, mtu mwingine angeweza kusema kwamba tungewaacha tu ili wakawe
mambumbumbu waweze kutawalika vizuri kwa hiyo tukaaongeza idadi ya
wanafunzi wanaoingia darasa la kwanza"
Rais
mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini Mkapa miezi kadhaa iliyopita
aliwahi kusikika akisema kuwa kuna haja ya kuwa na mjadala wa kitaifa
kuhusu elimu ya Tanzania kwa madai kuwa kuna unadhaifu mkubwa na
kushukwa kwa kiwango cha elimu ya Tanzania.