-->

MBEYA: Mwanafunzi wa Chuo ajinyonga kufuatia matokeo ya mpira Kombe la UEFA


  1. IMG_20180527_152357_394.jpg
    New
    Kijana wa Chuo cha S. Agustine Mbeya amekutwa akiwa amejinyonga kwa kile ambacho tetesi zinazotaja ni kwa sababu ya matokeo ya mpira katika mtanange wa Kombe la UEFA, baina ya Real Madrid na Liverpool.

    Pichani ni baadhi ya majirani wa Kijana huyo pamoja na uongozi wa Serikali za mtaa wa maendeleo uliopo jijini Mbeya wakiambatana na Jeshi la Polisi muda huu kuupeleka mwili huo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

    Habari kamili kuhusiana na tukio hilo, zitafuata baada ya ripoti rasmi. 

    ======

    Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo cha Saint Agustine Mbeya, Moses Mashaka amejinyonga kwa mujibu wa mashuhuda wa eneo analoishi wamesema Mwanafunzi huyo alikuwa shabiki Klabu ya Liverpool na inadaiwa kuwa kitendo cha kufungwa kwa Klabu hiyo goli 3-1 ndio sababu.

    Hata hivyo wengine wamesema Mwanafunzi huyo alijiingiza katika mchezo wa Kamari maarufu kama Betting na kitendo cha kuliwa inawezekana ikawa sababu

    Akithibitisha kutokea kifo hicho Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Mussa Taibu amesema ni kweli amejinyonga kwa kutumia kanga chumbani kwake na aliyegundua kuwa kujinyonga ni Baba mwenye nyumba.

Read also-: