Mmiliki wa Facebook ameomba radhi kwa watumiaji wote wa mtandao huo
Mwanzilishi
wa mtandao maarufu duniani wa Facebook, Mark Zuckerberg, kwa mara ya
kwanza tangu kuzuka kwa kashfa ya Cambridge Analytica, inayotuhumiwa
kuingilia data za watumiaji milioni 50 wa mtandao huo, ameibuka na
kudai kwamba wamefanya makosa.
Katika
ujumbe wake kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zuckerberg bila kuomba
radhi kwa kile kilichotokea, amesema kitendo hicho kimewavunjia
uaminifu. Hivyo kutokana na hali hiyo ameahidi kufanyika mabadiliko
kadhaa ili kutoingiliwa wala kudukuliwa kwa taarifa za watumiaji wake.
“Tuna
wajibu wa kuzilinda taarifa zenu na kama tukishindwa kuzilinda hatuna
sifa ya kuwahudumia, mimi ndiye niliyeanzisha mtandao huu wa Facebook,
mwisho wa siku ninawajibika kwa chochote kinachotokea katika mtandao
wetu,” amesema Zuckerberg.
Katika kufuatilia matatizo ya sasa na ya zamani amesema atafanya mambo yafuatayo;
- Kuchunguza mitandao yote ambayo inashirikiana na uga wa Facebook kabla ya kufanyiwa mabadiliko ya mwaka 2014 ya namna ya kuweza kupata taarifa ya watumiaji.
- Kufanyia uchunguzi kazi za programu za kimitandao zinazotiliwa shaka.
- Kupiga marufuku mwanzilishi wa programu yoyote ambayo inagoma ama haitoi ushirikiano katika uchunguzi pamoja na hatua nyingine ambazo wanaona zitafanya Facebook kuwa mahali salama.