Na Ripota Wetu,Globu ya jamiiMKURUGENZI Mtendaji wa
Kampuni ya Wakala ya Vyuo Vikuu vya Nje ya Darwin, Joseph Makungu
amesema mfumo mpya wa hati ya kusafiria unapaswa kuwangalia wanafunzi
wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya nje ambao hawana sifa ya kupata hati
hiyo kutokana kutofikisha miaka 18 ya kuweza kupata hati hizo.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi huyo amesema mamlaka zinazotoa
vitambulisho ni vema kuangalia kundi hilo ili kupata hati ya kusafiria
pale wanapohitaji kwa ajili ya masomo katika vyuo vikuu vya nje.
Amesema
hati ya kusafiria ambayo imeanza kutolewa ni ya viwango vya kimataifa
ambapo Tanzania imeweza kuthubu katika kwenda na wakati.
Makungu
amesema wakala wa vyuo vikuu vya nje kutokana na mfumo wa hati ya
kusafiria kwa idara ya uhamiaji kuweza kuwapa elimu juu ya mfumo
wakaulewa ili mbele ya safari wasipate usumbufu kwa wanafunzi pale
wanapotaka kusafiri kwa masomo katika vyuo vikuu vya nje.Mkurugenzi
Mtendaji Kampuni ya Uwakala wa Vyuo Vikuu vya Nje, Joseph Makungu
akizungumza na waandishi habari kuhusiana na mfumo wa Hati ya Kusafiria,
jijini Dar es Salaam.