Zaidi ya wanafunzi elfu 30 wakosa udahili elimu ya juu mwaka huu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako
Zaidi ya wanafunzi elfu thelathini walioomba kujiunga na masomo ya elimu
ya juu nchini wamekosa udahili baada ya kushindwa kukidhi vigezo
vilivyowekwa na mwisho wa udahili ni hii leo saa sita usiku
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako
amesema hayo katika mahojiano maalumu TBC ambapo amevionya vyuo
vilivyofungiwa udahili kutodahili wanafunzi.
Kuhusu utayari mazingira wezeshi kwa wanafunzi wenye ulemavu katika
shule mbalimbali, serikali imekiri bado mazingira siyo wezeshi hususani
katika shule za msingi.