TCU: AWAMU YA TATU YA UDAHILI-KWA WALIOKOSA AWAMU YA KWANZA NA YA PILI
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)
TAARIFA KWA UMMA
Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa Awamu ya Pili ya Udahili wa
wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na masomo ya shahada za awali ulimalizika
tarehe 10 Oktoba 2017. Kutokana na waombaji wengi kutochaguliwa kwa sababu
mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa Awamu ya Tatu kuanzia
tarehe 16 hadi 18 Oktoba 2017. Tume
inapenda kusisitiza yafuatayo:
a) Awamu
hii itawahusu waombaji waliokosa nafasi kwenye Awamu ya Kwanza na ya Pili
kutokana na ushindani au kukosa sifa katika programu walizoomba;
b) Waombaji
waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja; wanatakiwa kuamua mara moja kwa kuchagua
chuo kimoja tu na hatimaye kukiarifu chuo husika;
c) Awamu
hii haitawahusu waombaji wapya (ambao
hawajawahi kutuma maombi katika
awamu mbili zilizopita);
d) Waombaji
ambao hawatathibitisha uchaguzi wao au kujithibitisha zaidi ya chuo kimoja
hawatatambuliwa na Tume katika udahili wa mwaka 2017/18
e) Waombaji
kuwasiliana moja kwa moja na mara kwa mara na vyuo husika kwa masuala yote
yanayohusiana na zoezi la udahili badala ya kuja TCU.
f) Waombaji
wote kutembelea Tovuti za vyuo ili kufahamu hatima ya maombi yao. Aidha, Tume
inapenda kusisitiza kuwa utaratibu wa kutuma maombi na kuthibitisha ni ule ule
uliotumika katika awamu mbili zilizopita za Udahili.
Imetolewa na
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
16 Oktoba 2017