kali jopo la walimu wakimbia wakati wa uhakiki wa vyeti tanzania kutokana na vyeti vyao kuwa feki
BAADHI ya walimu nchini wamekimbia vituo vyao vya kazi kutokana na uhakiki wa vyeti unaoendeshwa na serikali, kubaini watumishi hewa na wale wasiokuwa na sifa kwa kukosa vyeti halali vya kitaaluma.
Hape alisema wamepata taarifa kuwa baadhi ya walimu waliokuwa wakifanya kazi pasi na sifa za utumishi huo kuyakimbia maeneo yao ya kazi kutokana na serikali kuendesha zoezi la ukaguzi wa vyeti kwa watumishi wa umma.
Hata hivyo, alisema kwa sasa bado hawajapata idadi maalumu ya walimu ambao wamekimbia zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma, lakini mara tu litakapokamilika, watapata idadi kamili ya walimu hao waliokimbia vituo vyao.