JWTZ LASEMA LIKO IMARA KULINDA MIPAKA YA NCHI
jeshi la wananchi Tanzania (jwtz) limewahakikishia watanzania kuwa liko imara katika kulinda mipaka ya nchi huku likisema limekwisha kujiimarisha kimfumo na kivifaa ili kuhakikisha wananchi wake wanakuwa salama nyakati zote
kauli hiyo ya jwtz imetolewa dar es salaam na mnadhimu mkuu wa jwtz luten canal venance mabeyo dakika chache baada ya kufungua mafunzo maalumu ya namna ya vikosi vya jwtz vitakavyoweza kukabiliana na adui keenye fukwe na visiwa vilivyo ndani ya bahari mafunzo hayo ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya jwtz yameshirikisha vikosi vya anga , nchi kavu na baharini ikiwa ni pamoja na askari wa akiba mafunzo hayo yanatarajiwa kufikia tamati septemba 30 mjini bagamoyo ambapo amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ambaye pia ni rais wa tanzania dkt. John magufuli atahitimisha mafunzo hayo mkuu wa mafunzo ya kivita jeshini meja jenerali issa nassoro amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kuwajengea uwezo wapiganaji wa jwtz hasa katika kipindi hiki ambacho jeshi limejiimarisha kivifaa huku kaimu mkuu wa kamati ya wanamaji akisema wako imara katika kulinda mipaka yote ya bahari na kuwataka watanzania kutokuwa na hofu yeyote kwani wako salama