Serikali Yapandisha Mishahara kwa Watumishi 59,967
Rais
John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa serikali ya awamu ya tano
imewapandisha vyeo na kurekebisha mishahara ya watumishi 59,967 baada
ya zoezi la uhakiki wa vyeti feki hewa kukamilika.
Rais
Magufuli amesema hayo leo kwenye sherehe za maazimisho ya mbio za
Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu za miaka 18 ya kifo cha Baba wa Taifa
Mwalimu Nyerere, sherehe ambazo zimefanyika visiwani Zanzibar.
Rais
Magufuli katika hotuba hiyo alitolea mfano uzalendo wa Baba wa Taifa
ambaye aliamua kupunguza mshahara wake na kukataa kuongeza mishahara ya
watumishi wachache huku walio wengi wakipata shida.
“Ninaposema
hivyo simaanishi kuwa mishahara isiongezwe. La hasha. Ninachosema ni
kwamba kabla ya kudai nyongeza ya mishahara ni lazima kwanza kufahamu
uwezo wa Serikali, lakini pia tutambue kuwa kuna Watanzania wenzetu
wengi tu wanaohitaji kuboreshewa huduma.
"Hata
hivyo baada ya kukamilisha zoezi la uhakiki wa watumishi hewa na vyeti
feki, Serikali imewapandisha vyeo na kuwarekebishia mishahara watumishi
59,967 ambapo kiasi cha Shilingi Bilioni 159.33 zimetengwa kwenye bajeti
ya mwaka huu na mishahara mipya itaanza kulipwa kuanzia mwaka huu. Na
kwa upande wa Zanzibar kima cha chini cha mshahara kimeongezwa kutoka
Shilingi 150,000/- hadi kufikia Shilingi 300,000/-” Amesema Mhe. Rais
Magufuli.
Mbali
na hilo Rais Magufuli aliwataka vijana kuendelea kujielimisha katika
mambo mbalimbali na kuwataka kutojihusisha na masuala ya madawa ya
kulevya na kujikinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI